Wananchi wenye hasira kali wamejichukulia sheria mkononi kwa kulichoma gari aina ya Lori baada ya dereva wake kumgonga na kufa papo hapo muuguzi wa Zahanati ya Kaseme Wilayani Geita.

Tukio hilo limetokea Jana usiku katika Kijiji cha Kaseme wakati marehemu huyo akiwa katika Bodaboda pamoja na watoto wake wawili, mmoja amefahamika kwa jina Paulo Tarafa mwenye miaka 3 na mwingine mchanga wa miezi miwili ambao wao wamenusurika na kifo hicho.

Aidha, mashuhuda wa tukio hilo wamesema lori hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi na walipojaribu kupishana na gari jingine ndipo likawagonga na mama huyo kuumia kuanzia sehemu ya kiuno hadi miguuni na kusababisha utumbo kutoka nje.

Wamesema kuwa sababu kubwa iliyochangia watoto hao kutopatwa na madhara kama marehemu mama yao ni kwa kuwa alikuwa amewapakata kifuani ambako hawakuguswa na gari hilo.

Hata hivyo, Jina la marehemu ni Martha Paulo ambaye mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha maiti kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Geita.

Video: Abdul Nondo alijiteka mwenyewe- Kamanda Mambosasa
Al Ahly yatangazwa bingwa wa Misri kabla ya ligi kumalizika

Comments

comments