Gavana wa Mexico ambaye aliapishwa mwezi huu, Martha Erika Alonso na mumewe ambaye ni Seneta, Rafael Moreno Valle wamefariki dunia baada ya helikopta waliyokuwa wamepanda kuanguka, Jana majira ya mchana.

Helikopta hiyo iliyokuwa imewabeba viongozi hao wa Serikali ambao ni wanandoa ilianguka muda mfupi baada ya kuanza kupaa, kwa mujibu wa ripoti ya BBC.

Katika ajali hiyo, marubani wote wawili walipoteza maisha pamoja na abiria mwingine aliyekuwa akisafiri pamoja na wanandoa hao.

Mamlaka zimeeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo kinaweza kuwa kushindwa kufanya kazi kwa ufasaha kwa baadhi ya mifumo ya chombo hicho. Uchunguzi rasmi umeanza ili kubaini chanzo halisi.

Alonso mwenye umri wa miaka 45 aliapishwa Desemba 14 mwaka huu kama Gavana wa jimbo la Puebla, kufuatia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.

Mumewe, Moreno mwenye umri wa miaka 50 aliwahi kuwa Gavana wa jimbo hilo kati ya mwaka 2011 na 2017, kabla ya kuwa Seneta.

Waziri wa Ulinzi, Alfonso Durazo amesema kuwa helikopta hiyo waliyokuwa wameikodisha ilipoteza mawasiliano na kuanguka dakika kumi baada ya kuruka.

Jeshi latekeleza hukumu kwa kumuua kwa risasi gaidi wa Al-Shabaab
Video: Moto wa JPM waibua wasomi, Kesi iliyofunguliwa kwa mbwembwe yailiza Serikali