Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Urlich Matei amethibitisha kutokea ajali ya gari hii leo Agosti 16, 2022 na kusababisha vifo vya watu wanane katika eneo la Shamwengo karibu na kituo cha mafuta Inyala mkoani humo.

Matei amesema, gari kubwa lililokuwa limebeba kontena la mchanga, lilifeli breki na kuligonga basi la Super Rojas, lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Njombe.

Amesema, baada ya kuligonga basi hilo liliendelea kushuka zaidi na kuligonga gari lingine aina ya benzi na kusababisha vifo na majeruhi, ambao idadi yao bado haikujulikana haraka.

“Waliopoteza maisha ni nane japokuwa bado idadi rasmi haijajulikana ila baadaye taarifa ya daktari itaeleza kwa ujumla, ila majeruhi wamesambazwa kwenye hospitali tofauti ikiwamo Igawilo na Mkoa,” amesema Matei.

Kamanda huyo amesema, chanzo kikubwa katika ajali hiyo ni kufeli breki kwa gari hilo na kubainisha barabara hiyo ni finyu, na kwamba tayari wameanzisha ukaguzi wa maroli yanayotumia njia hiyo.

Kenya: Raila akataa matokeo ya urais, asema hatakubali
Rais Samia awapongeza wakenya