Mamlaka za usalama nchini Ghana zimewakamata watu watatu wakiwa na vifaaa vya mlipuko na silaha nyingine za kivita wakidaiwa kupanga njama za kupindua Serikali ya Rais Nana Akufo – Addo.

Kwamujibu wa vikosi vya usalama katika Taifa hilo lililopo Afrika Magharibi, vimesema vilikuwa vikifuatilia shughuli za watuhumiwa hao kwa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kukamatwa ijumaa ya wiki iliyopita.

Watuhumiwa hao wamewekwa chini ya ulinzi wa kikosi cha pamoja cha usalama ambacho kinajumuisha idara ya ushauri wa ulinzi wa nchi, idara ya upelelezi wa jinai na ofisi ya upelelezi wa kitaifa ambapo  bado wanawahoji watuhumiwa wakati uchunguzi zaidi ukiendelea.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunakuja mwaka mmoja kabla ya nchi hiyo kuingia kwenye uchaguzi wa Rais ambapo Rais Nana anayemaliza muda wake anatarajiwa kugombea kwa muhula mwingine.

 

Lugha chafu yamponza Dimitri Payet
Video: Hawa ndiyo nyota wa Simba watakao ikosa mechi leo