Mgombea nafasi ya urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru watanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano wake wa kampeni za uchaguzi mkuu katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Magufuli ameelezea kufurahishwa na umati wa watu waliojitokeza  katika kampeni hizo kufuatia uwanja huo kujaa na wengine kushindwa kuingia ndani ya uwanja.

“Nasema ahsanteni sana, na huo ni ujumbe tosha kwa wale wanaojitokezatokeza, wataisoma namba,” amesema Magufuli.

“Na kilichonifurahisha zaidi, wananchi waliohudhurua hapa, pamoja na waliojaa nje, si wanaCCM tu, ni wa vyama vyote kwa sababu wanaamini katika maendeleo na maendeleo hayana chama” ameongeza Magufuli.

Awali wakati msanii Nassib Abdul maarufu diamond platnumz  akitumbuiza aliitwa jukwaani na JPM na kuvishwa kofia aliyokuwa ameivaa Magufuli.

Magufuli yuko mkoani Mwanza alipowasili jana kwa ajili ya mikutano ya kampeni zake kuomba ridhaa kuchaguliwa kuwa rais kwa muhula wa pili.

Azam FC waitambia Polisi Tanzania, Malale ajibu
Waandamana uchaguzi kucheleweshwa