Mitandao ya kijamii inaendelea kukumbwa na nyundo za sheria ya vizuizi zinazopelekea kufunguliwa kwa mashauri mengi mahakamani na kuwafunga baadhi ya watumiaji.

Serikali ya Ufaransa imewaonya wazazi nchini humo kuwa wanaweza kujikuta wakifungwa jela kwa kosa la kupost picha za watoto wao kwenye mtandao wa Facebook, kwa mujibu wa sheria mpya ya mtandao nchini humo.

Sheria hiyo inakataza wazazi kupost picha za watoto wao kwenye mitandao bila idhini ya watoto hao, hali ambayo inaonesha katazo la moja kwa moja kwani mtoto mdogo hana utashi wa kutoa ruhusa au kuzuia.  Wazazi watakabiliwa na faini hadi €45,000 au kifungo jela endapo watoto wao wataamua kuwashtaki watakapokuwa na utashi wa kutosha siku za usoni.

Profesa Nocola Whitton wa Chuo Kikuu cha Manchester Metropolitan ameiambia Guardian kuwa kwa mantiki hiyo kutakuwa na kesi nyingi zitakazofunguliwa na watoto wa sasa miaka mitano hadi kumi na tano ijayo.

“Nadhani kutakuwa na rundo la kesi miaka mitano ijayo kutoka kwa toto wa sasa hivi pale watakapokuwa na kubaini kuwa karibu maisha yao yote ya utotoni yaliwekwa kwenye mitandao ya kijamii. Wazazi wanapaswa kuwa makini hivi sasa… hawa watoto wanaweza wasipende walichofanyiwa kwa miaka ijayo,” alisema.

Prefesa Nocola amewasihi wazazi kutoendekeza tabia ya kupost picha za watoto wao kwenye mitandao ya kijamii hadi watakapofikia umri wa kuweza kujadili na kukubaliana nao.

Sitta awatetea wabunge wa Chadema
Uongozi Wa Simba SC Washinikizwa Kujiuzulu

Comments

comments