Orodha ya wachezaji 30 watakaowania tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu 2018 imekamilika, baada ya kutangazwa kwa mafungu kuanzia jana jumatatu.

Paul Pogba na Harry Kane ni miongoni mwa wachezaji wanaocheza kwenye ligi kuu ya England waliotajwa kwenye orodha hiyo, wakiungana na Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Luka Modric.

Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah, naye amejumuishwa kwenye orodha hiyo, huku kigezo kikubwa kilichombeba ni hatua ya kupachika mabao 32 katika ligi ya England msimu uliopita, na kuwa mfungaji bora.

Salah ameungana na wachezaji wenzake wa klabu ya Liverpool kama mlinda mlango Alisson, Roberto Firmino pamoja na Sadio Mane.

Hafla ya kumtangaza mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or kwa mwaka huu 2018, imepangwa kufanyika Disemba 03, nchini Ufaransa.

Orodha kamili ya wachezaji 30 waliotajwa kuingia katika kinyang’anyiro cha Ballon d’Or mwaka huu.

 1. Sergio Aguero (Manchester City, Argentina)
 2. Alisson (Liverpool, Brazil)
 3. Gareth Bale (Real Madrid, Wales)
 4. Karim Benzema (Real Madrid, France)
 5. Edinson Cavani (Paris Saint-Germain, Uruguay)
 6. Thibaut Courtois (Real Madrid, Belgium)
 7. Cristiano Ronaldo (Juventus, Portugal)
 8. Kevin De Bruyne (Manchester City, Belgium)
 9. Roberto Firmino (Liverpool, Brazil)
 10. Diego Godin (Atletico Madrid, Uruguay)
 11. Antoine Griezmann (Atletico Madrid, France)
 12. Eden Hazard (Chelsea, Belgium)
 13. Isco (Real Madrid, Spain)
 14. Harry Kane (Tottenham, England)
 15. N’Golo Kante (Chelsea, France)
 16. Hugo Lloris (Tottenham, France)
 17. Mario Mandzukic (Juventus, Croatia)
 18. Sadio Mane (Liverpool, Senegal)
 19. Marcelo (Real Madrid, Brazil)
 20. Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain, France)
 21. Lionel Messi (Barcelona, Argentina)
 22. Luka Modric (Real Madrid, Croatia)
 23. Neymar (Paris Saint-Germain, Brazil)
 24. Jan Oblak (Atletico Madrid, Slovenia)
 25. Paul Pogba (Manchester United, France)
 26. Ivan Rakitic (Barcelona, Croatia)
 27. Sergio Ramos (Real Madrid, Spain)
 28. Mohamed Salah (Liverpool, Egypt)
 29. Luis Suarez (Barcelona, Uruguay)
 30. Raphael Varane (Real Madrid, France)
Wapenzi wakutwa na viungo vya miili ya binadamu
Uhaba wa walimu wamchefua Majaliwa

Comments

comments