Watanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kabla ya kufanya maamuzi ya kuweka fedha zao katika mfumo wa fedha zilizo kwenye mfumo wa bitcoins kuepuka majanga ya kiuchumi.

Tahadhari hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Hazina na Masoko wa Benki ya CRDB, Alex Ngusaru alipokuwa akizungumza na wanahisa wa benki hiyo wikendi iliyopita.

Ngusaru aliwataka Watanzania kufikiria mara mbili kabla ya kuchukua uamuzi wa kujiunga na mfumo huo kutokana na msimamo wa thamani yake kupanda na kushuka kwa kasi.

“Uamuzi wa kujiunga unabaki kwa mtu anayependa kufanya hivyo. Hata hivyo, ninapenda kuwashauri kuwa wekezeni kwenye Bitcoins pale tu mnapokuwa na fedha za ziada,” alisema Ngusaru.

Kupanda na kushuka kwa thamani ya ‘Bitcoins’ kati ya mwezi Disemba mwaka jana kulikuwa na picha ya tofauti kubwa ambayo wataalam wa uchumi waliiona kama changamoto. Disemba, Bitcoin moja ilikuwa sawa na $20,000 (sawa na sh. 44.4 milioni za Tanzania). Lakini mwezi Machi, thamani ya Bitcoins moja iliporomoka hadi $7,000 (sawa na sh. 159 milioni za Tanzania) na baadaye ikapanda hadi $8,000 (sawa na sh.190 milioni).

Mtaalam huyo alisema kuwa kupanda na kushuka kwa thamani ya Bitcoins hutegemea zaidi tetesi zilizopo, hali ambayo alisisitiza, “hili siyo eneo zuri zaidi la kuwekeza fedha zako kama hauna fedha za ziada.”

Mwaka jana, aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu alisema kuwa Watanzania wanaojihusisha na Bitcoins wanafanya hivyo kwa matakwa yao na watahusika na madhara yote wao wenyewe.

Mfumo huo wa kifedha ambao umesambaa katika nchi mbalimbali, haudhibitiwa na mfumo wowote wa Serikali. Zipo nchi kadhaa ambazo zina ‘ATM za kutoa Bitcoins’ na hata kubadilishana mali na mahari kupitia mfumo huo.

Mwaka jana nchini Kenya, familia moja ilikubali kumuoza binti yao na kupewa Bitcoins iliyokuwa na thamani husika.

Maduro ashinda uchaguzi Venezuela, wapinzani wapinga matokeo
Video: Moto waanza kuwaka kiti cha Mbowe Chadema, Ukweli ulinzi ukuta Mirerani