Je unafahamu kuwa katika mahusiano endapo mwanamke/mwanaume ni mchepukaji basi mtu wa namna hiyo huwa hivyo daima, kwa lugha ya kingereza wanasema ”Once a Cheater always a cheater”.

Na hii ndio sababu ya mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Zari The Boss Lady kuachana na baba mtoto wake, Diamond Platinumz aliyemsaliti kimapenzi na kumzalisha mwanamke mwingine na kuamua kujitoa katika mahusiano hayo.

Kuchepuka kwa tafsiri rahisi na iliyozoeleka inamaanisha mtu anayekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na zaidi ya mtu mmoja, hivyo humdanganya yule aliyenaye njia kuu.

Kuchepuka ni tabia ya mtu japokuwa wengi hutetea jambo hilo wakidai kuwa kuchepuka husababishwa na jambo fulani katika mahusiano.

Kwa mtazamo wangu kuchepuka ni tabia ya mtu inayotokana na kuendekeza tamaa za mwili ndio maana baadhi ya wanasaikolojia juu ya mahusiano wamethibitisha hilo kuwa ”once a cheater always a cheater”.

Wanaume/wanawake wengi hutoa sababu ya kuchepuka wakidai kuwa hawaridhishwi na mwenendo wa mahusiano yao, au matatizo mengine lakini ukweli ni kwamba mchepukaji ni mchepukaji haijilishi anaridhishwa au haridhishwi.

Kwani wapo wanaume/wanawake ambao wanakutana na matatizo kama hayo katika mahusiano lakini hawatatui tatizo hilo kwa kufanya udanganyifiu katika mapenzi bali hutafuta njia mbadala itakayo ua tatizo na sio kuongeza tatizo, kwani endapo mtu atafanya udanganyifu katika mahusiano mengi yanatarajiwa kutokea yakiwemo mimba zisizotarajiwa na za nje ya ndoa, magonjwa ya zinaa, ugomvi na n.k

Hivyo Wanaume/wanawake ni wakati sasa wa kupenda familia/mahusiano kwa kuzijali na kukinzana na tamaa za mwili matatizo katika familia au mahusiano hayazuiliki hivyo yatatutiliwe kwa njia sahihii na si vinginevyo.

Nini maoni yako.

Kilimo cha umwagiliaji kutatua changamoto za mabadiliko ya Tabianchi
IMF yaonya kuhusu sera za Marekani