Wanasayansi wa Shirika la Anga za Juu la Marekani (NASA) wametangaza kugundua sayari ya ukubwa wa Dunia ambayo ina uwezekano wa kuwa na miamba na watu kuweza kuishi.

Sayari hiyo inayoitwa TOI 700 e, ni ndogo kuliko Dunia na inazungukwa na nyota ndogo nyekundu inayoitwa TOI 700 iliyo umbali wa miaka 100 ya mwanga ikiwa ni mojawapo ya sayari nne zinazozunguka nyota, pamoja na TOI 700 b, c na d.

Sayari aina ya TOI 700 e, iliyogunduliwa na Wanasayansi ambayo ni ndogo kuliko Dunia. Picha ya KFOR 1240.

TOI 700 d, ilikuwa tayari inajulikana kuwa katika eneo linaloweza kukaliwa na binadamu na ugunduzi wa Satellite ya NASA (Transiting Exoplanet Survey), ambayo hufuatilia sehemu kubwa za anga kwa siku 27 ili kujua mabadiliko wa mwangaza wa nyota unaosababishwa na sayari.

Hata hivyo, imechukua zaidi ya mwaka mmoja kwa wanasayansi kugundua TOI 700 e, na kubaini ilikuwa ndani ya eneo la nyota inayoweza kukaliwa na binadamu ambapo ugunduzi wake uliwasilishwa katika Jumuiya ya Wanajimu ya Marekani huko Seattle.

Robertinho: Sikuwa na maana mbaya
Ahmed Ally afichua mazungumzo ya Mo Dewji