Katika kuhakikisha kuwa elimu kuhusu mazingira inawafikia wananchi na kukabiliana uharibifu wa mazingira unaoendelea nchini, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari amesema kuwa kuna umuhimu wa kujenga uelewa kwa Maafisa Sheria, forodha na Wakaguzi wa mazingira na ubora wa viwango nchini ili waweze kutambua kemikali na taka hatarishi kwa mazingira na matumizi  ya Binadamu.

Ameyasema hayo mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa  Warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, ambapo amesema kuwa changamoto kubwa ambayo inaikabili dunia kwa sasa ni usimamizi wa taka hatarishi katika jamii.

”Hizi kemikali na taka zinahitajika kusimamiwa vizuri ili kupunguza madhara ya afya kwa binadamu na mazingira na pia Wanawake na watoto wapo kwenye hatari kubwa ya kuathirika na kemikali hizo,” amesema Tandari.

Aidha, Tandari amewataka Maofisa walioalikwa kujengewa uelewa wa kemikali na taka hatarishi wakaitumie elimu hiyo katika majukumu ya kazi zao za kila siku  na hivyo kupelekea usimamizi stahiki wa wa taka na kemikali hizo.

Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais – Idara ya Mazingira ili kuwajengea uelewa Maafisa hao waweza kudhibiti uingizwaji  na usambazaji wa kemikali hizo hatarishi Nchini.

Hata hivyo, Katika Warsha hiyo Maafisa wa forodha, sheria na wakaguzi wa Mazingira na viwango vya ubora wamehudhuria hivyo basi uelewa juu ya kemikali hizo utaongezeka na utawasaidia katika majukumu yao ya kila siku wanapokua makazini.

Hongera Linah Sanga kwa kabinti
Marry Majaliwa awafunda wanafunzi wa kike nchini