Idadi kubwa ya wanawake waliofika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kuwa wanaume waliozaa nao wametelekeza watoto, wamewataja wabunge na viongozi wa dini.

Hatua hiyo imewekwa wazi jana na Makonda mbele ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa chanjo ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake iliyofanyika Mbagala mkoani humo.

“Kati ya wanawake 480 waliofika katika ofisi yangu, kati yao 47 wamesema wametelekezwa na wabunge huku 14 wakieleza wametelekezwa na viongozi wa dini,” Makonda anakaririwa.

Mkuu huyo wa mkoa aliwakosoa wanaobeza hatua hiyo aliyochukua na kuwaeleza kuwa ameongeza siku ili aweze kuwasaidia wanawake wengi zaidi.

Amesema wanaomkosoa wanadai hilo sio jukumu lake bali ni kazi ya Ustawi wa Jamii.

Katika timu yake, wanawake waliofika katika ofisi zake wanasikilizwa na wanasheria, watumishi kutoka Ustawi wa Jamii pamoja na dawati la wanawake la polisi.

Youssef Msakni azusha hofu Tunisia
Video: Barcelona yang'olewa UEFA

Comments

comments