Mchambuzi wa Siasa, Ibrahim Jeremiah amewataka wanasiasa kuangazia sera zitakazoweza kubadilisha maisha ya wananchi na kuacha kupambana na Hayati Rais Magufuli ambaye hayupo kwasasa na hawezi kujibu hoja za wanaombeza.

Jeremiah ameyasema hayo hivi karibuni katika mahojiano maalum na Dar24 Media, kuhusu mwenendo wa masuala ya kisiasa nchini.

Mchambuzi wa siasa, Ibrahim Jeremiah.

Amesema, “hakuna aliyewahi kupambana na Marehemu akashinda zaidi ya kuonekana hayupo timamu, tutengeneze sera na mikakati itakayoweza kututoa hapa tulipo ili Watanzania waweze kupata unafuu wa maisha.” Amesema Jeremiah.

Aidha, ameongeza kuwa wapo baadhi ya wanasiasa wakiwemo wa Chama tawala na upande wa upinzani ambao hutumia muda wao mwingi kwenye majukwaa kumkosoa Hayati Magufubadala ya kuelezea mikakati mbadala ya kuindeleza Tanzania kisera na kiuchumi.

Simba SC yamkataa Ibourahima Sidibé
Young Africans: Tutaisambaza US Monastir