Biashara ya ngono inadaiwa kukithiri mkoani Iringa huku ikihusisha wanaume wanaofanya mapenzi ya jinsia moja maarufu kama ‘mashoga’.

Taarifa kutoka mkoani humo zimeeleza kuwa zaidi ya wanaume 1500 wamejitokeza hadharani na kujitangaza kuwa ni mashoga na wanafanya biashara ya ngono huku idadi hiyo ikiongozwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliofika mkoani humo kutafuta elimu.

Imeelezwa kuwa tamaa ya starehe na vitu vya gharama kubwa zaidi ya uwezo wao wa kifedha ni chanzo kikuu cha vijana hao wa kiume kujiingiza katika biashara ya ngono wakijiuza kwa wanaume wenzao.

Kutokana na hali hiyo, Shirika la Restless Development chini ya mradi wao wa kusaidia afya ya uzazi na makuzi kwa vijana unaojulikana kama Dance For Life, limepanga kuwakutanisha wanafunzi wa vyuo hivyo na uongozi wa vyuo hivyo ili kuwasaidia wanafunzi hao kujinasua katika mchezo huo mchafu na haramu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Star TV, Serikali inaona kuwa tatizo hilo la Ushoga linaweza kumalizwa na jamii yenyewe endapo wazazi na walezi watakemea mapema tabia na mienendo hatarishi ya watoto wao.

Cristiano Ronaldo Kutundika Viatu vya Soka Akiwa Real Madrid
Nape Atolea Majibu Taarifa Ya kupiga Marufuku Vimini, Mlegezo