Kama ilivyozoeleka mara nyingi mwanamke aliyeolewa akikosea huadhibiwa na mume wake kwa kipigo, lakini hii sio desturi ya watu wengi kwa sasa maana wanasema ukiona mwanaume ananyosha mkono kumpiga mke wake ujue huyo mwanaume hakuwahi kunyosha mkono kujibu swali darasani, mambo yamebadilika zama hizi.

Ambapo wanawake mkoani Rukwa wameanzisha utaratibu mpya wa kugawa vipigo vikali na mashambulio na kuwajeruhi  waume zao kutokana na tabia zao za ubahili wa kutoacha fedha za matumizi nyumbani na kurudi wakiwa wamelewa.

Ambapo mwanaume mmoja mkoani humo amenusurika kifo baada ya kupokea kipigo cha kufa mtu na mke wake, ambapo mwanamke huyo baada ya kumpiga aliamua kumchoma kisu mumewe.

Tukio hilo limetokea juzi ambapo imeelezwa kuwa mwanaume uyo alirudi nyumbani  akiwa amelewa pombe za kienyeji na kuanza kumlazimisha mkewe amuandalie chakula, ndipo mwanamke  huyo alipoamua kuchukua hatua mkononi kwa kumuadhibu mumewe kwa kumchapa na kumchoma na kisu.

Mashahidi waliokuwepo wameeleza kuwa walisikia majibizano baina ya wawili hao ambapo inasemekana kuwa mwanamke huyo alichukua uamuzi huo baada ya kupandwa na hasira kwani imekuwa tabia ya mume wake kutoacha fedha za matumizi nyumbani na kuwasili nyumabani akiwa amelewa na kudai chakula.

Aidha Serikali ilingilia kati suala hilo na kusema  ‘Kama serikali ya kijiji tunalaani tabia hiyo ya wanawake kuwadhalilisha waume zao wa ndoa, tabia ambayo imeanza kushamiri wilayani hapa’’ amesema Ofisa mtendaji wa kijiji, Daniel Kalumbilo.

Hata hivyo Kalumbilo amesema kuwa tukio hilo si mara ya kwanza kutokea kijijini hapo.

Pia baadhi ya wanaume walio kwenye ndoa wamekiri kunyanyaswa na wake zao na kulaani vikali mashambulio hayo yanayofanywa na wake zao kijijini hapo.

 

CCM ‘wamrudia’ Maalim Seif kuhusu kubadili uongozi Zanzibar
Wachezaji wamgomea Trump, wapinga vikali agizo lake