Imeelezwa kuwa wanaume wenye Virusi vya UKIMWI (VVU) wanaongoza kwa kufa kutokana na kusuasua kunywa dawa za kufubaza virusi hivyo ikilinganishwa na wanawake.

Akitoa Taarifa katika  katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibitibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk.Leonard Maboko, amesema wanaume wamekuwa nyuma katika kupima Ukimwi na wanaojitokeza kupima wanapobainika kuwa na maambukizi wamekuwa hawanywi dawa hizo na hivyo hufariki.

Amefafanua kuwa takwimu za mwaka 2019 zinaonesha kuwa wanaume wanaoishi na VVU ni 628,830 huku wanawake ni 983,471. Hata hivyo, amesema vifo vinavyotokana na ugonjwa huo kwa wanaume ni 12,225 huku wanawake ni 9,304.

Amesema idadi ya wanawake wanaokufa ni ndogo kutokana na kuzingatia masharti ikiwemo kuanza kunywa dawa mapema pindi wanapobainika kuwa na ugonjwa huo.

Simba SC kama Arsenal, kuvaa jezi maalum 'VISIT TANZANIA'
Ibenge: Simba SC imejiandaa vizuri