Matukio ya watu kujiua nchini yanazidi kuongezeka kwani takribani watu 333 wamejiua katika kipindi cha mwaka 2016 hadi juni mwaka huu.

Takwimu zilizo tolewa na Naibu kamishna wa polisi (DCP), Adriane Magayane kwa niaba ya mkuu wa jeshi la polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro zinaonyesha kuwa mwaka 2016 wanaume walio jiua walikuwa 106 huku wanawake wakiwa 25, mwaka uliofuata 2017 wanaume walio jiua walikuwa 81 (92%) na wanawake 7(7.95%)

Aidha, uchunguzi uliofanywa kupitia machapisho mbalimbali unaonyesha kuwa wnawake wanaongoza kwa matukio ya kutaka kujiua kuliko wanaume lakini wnaume wanaongoza kwa kufanikiwa kujiua kuliko wanawake.

Vitendo vya watu kujiua kwa kujinyonga vinaongoza nchini, vikifuatiwa na matumizi ya sumu, risasi na kwa kutumia kisu. takwimu hizo za kipolisi zinabainisha kuwa katika mwaka 2016 watu 131 walijuia huku 101 wakijinyonga na 30 walitumia sumu, 2017 watu 88 walijiua 71 kwakujinyonga,16 kwa sumu na mmoja kwa risasi.

Katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu matukio ya watu kujinyonga yameongezeka kutoka 71 mwaka 2017 hadi 90 yakifuatiwa na matumizi ya sumu kujiua (21),Mkoa wa mwanza ndio kinara kwa kuwa na matukio (29) ukifuatiwa na mbeya matukio( 18), Dodoma (11), Tabora (11) na shinyanga(8)

Kwa upande wa mwnasaikolojia,kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP),Engelbert Kiondo amebainisha miongoni mwa sababu zinazo pelekea watu kijiua ni Utamaduni kwani kuna baadhi ya jamii zinazo amini kimakosa kuwa kwa mwanaume kujinyonga ni ujasiri.

Muro aanza kuwashughulikia vigogo waliopiga bilioni 3 za Kanisa
Tiwa Savage aweka rekodi tuzo za ‘MTV EMAs’