Leo nchini Finland kumefanyika mashindano yaliohusisha wanaume kuwabeba wake zao mabegani na kukimbia nao katika mazingira tofauti tofauti ikiwemo kuruka vikwazo mbalimbali na mchezo huo unaojulikana kama ”Wife Carrying Championship”.

Ni mashindano ya 23 tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo yaliyofanyika katika mji mdogo wa Sonkajarvi ambao una wakazi takribani 4,200 na kuhudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo wageni kutoka sehemu mbalimbali.

Mashindano hayo yamehusisha Jumla ya familia 53 (mke na mume) ambazo zilishiriki katika shindano hilo ambalo lilishirikisha nchi 13 zikiwemo Marekani, Uingereza, Estonia, Sweden na Lithuania.

Kwa mwaka huu Vytautas Kirkliauskas na Neringa Kirkliauskiene wameibuka na ushindi kutoka nchi ya Lithuania.

“Nafikiri kwa sababu tuna miezi mitatu pekee ya kuona mwanga tunahitaji kuwa na mashindano kama haya katika kipindi hiki na tunahitaji kumuonyesha kila mmoja uwezo wetu“, amesema  mmoja wa washiriki wa shindano hilo.

Wazo la kuanzisha shindano hilo lililetwa mnamo karne ya 19 na Ronkainen the Robber ambaye aliwashawishi vijana wenzake kubeba kati ya gunia la mbegu ama kumbeba nguruwe na kukimbia naye.

Video: Sheria 6 zitakazokufanya ushindwe kuishi Korea Kaskazini
Watatu mbaroni kwa wizi wa meno ya tembo