Mwanamke akifikia umri wa kuweza kuzaa uzazi wake hunyemelewa na matatizo kadha wa kadha, wengi huwawia vigumu kutambua hali zisizo za kawaida pindi wakiwa kwenye siku zao, ukweli  ni kwamba hedhi si ugonjwa ila kuna baadhi ya dalili unapaswa kuwa nazo makini na si kuchukulia kawaida.

Wengi wamezoea kwa jina la Fibroids huu ni uvimbe katika mfuko wa kizazi unaoota na kukua kwenye mfuko wa uzazi (uterasi). Majina mengine ya uvimbe huu ni uterine fibroids, myomas, au fibromyomas. Mara nyingi ugonjwa huu kwa takribani 99% hauna madhara kiafya na wala kuhusiana na ugonjwa wa kansa.

Dalili za ugonjwa huu; Kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku zako za hedhi, au kutokwa na damu kwa muda mrefu , na kutokwa na damu kusiko kwa kawaida katikati ya siku za mwezi, Mauvimu ya nyonga (uvimbe kugandamiza kwenye viungo vya nyonga) Kupata haja ndogo mara kwa mara, Maumivu ya mgongo, Maumivu wakati wa tendo la ndoa Upungufu wa damu kwa sababu ya kutokwa na damu kwa wingi wakati wa siku  Maumivu ya kichwa, Maumivu kwenye miguu Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo (Fibroids kubwa) Uzazi wa shida, Mimba za shida au  Kutopata mimba kabisa Kutoka kwa mimba mara kwa mara.

Ukikutana na dalili kama hizo juu wahi hospitali kwa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi.

Inakadiriwa kuwa kati ya asilimia 20 hadi 50 ya wanawake walio katika umri wa kuzaa, miaka 30 hadi 50, wana fibroids ingawa wengi wao hawahangaiki kuchukua vipimo vya fibroids. Uvimbe wa fibroids unakuwa na ukubwa tofauti tofauti, unaweza kuwa mdogo kama haragwe au kufikia ukubwa wa tikiti maji.

Sababu hasa za kuota kwa fibroids katika viungo vya uzazi vya mwanamke bado hazieleweki vizuri ingawa inaamika kwamba kila uvimbe wa fibroid unatokana na seli ya musuli wa uterus ambayo imeamua kuwa na tabia ya tofauti na nyingine na ikaanza kukua kwa haraka ikichangiwa na uwepo wa homoni ya estrogen.

Utafiti umeonyesha pia kuwa idadi ya wanawake wanaopatwa na fibroids katika kundi la wanawake ambao wamezaa watoto angalau wawili wakiwa hai huwa ni nusu ukilinganisha na wale ambao hawajazaa hata mara moja.

Wabunge wa Jubilee wataka jaji mkuu ang'oke
Watu wawili wauawa na jeshi la polisi