Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto amezindua Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika taasisi hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Kumbilamoto  amewataka wanawake waliopo katika sekta za nishati kujiamini na kufanya kazi kwa weledi huku wakitakiwa kutokukata tamaa ili kuweza kukuza sekta ya nishati hapa nchini.

Aidha ameahidi kuwa mstari wa mbele kuisaidia taasisi hiyo ambayo  imeonesha nia ya dhati kuinua wanawake katika sekta ya nishati na kuweza kutatua changamoto mbalimbali.

“Katika kuunga mkono TAWOE ameahidi kuisaidia taasisi hiyo katika kutatua changamoto zinazoikabili huku akiweka wazi kuwa tayari jiji limekwisha tenga asilimia Nne ya mapato yake kwenda kwa kina mama”. Amesema Kumbilamoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya TAWOE Mhandisi Gwaliwa Mashaka, amesema kupitia uzinduzi huo utasaidia kuwawezesha wanafunzi hasa wakike katika  kuonyesha kile wanachokifanya.

Nae mmoja wa washiriki ambaye ni mshauri muelekezaji masuala ya umeme  kutoka katika kampuni  ya Gein Energy  Product  Farm Dkt.Juliana Palangyo amesema wanawake wengi wapo katika sekta za nishati na wanajitahidi kwa weledi mkubwa huku changamoto kubwa ikionekana ni kutokukubalika.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto  akitazama baadh i ya teknolojia zinazofanywa kupitia nishati katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika Taasisi hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omari Kumbilamoto akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika Taasisi hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Taasisi ya TAWOE Mhandisi Gwaliwa Mashaka akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Taasisi ya Mtandao wa Wanawake kwenye Sekta ya Nishati (TAWOE) na programu mpya zilizopo katika Taasisi hiyo iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Bocco: Tukipongezwa na Mashabiki tunaumia
Waziri Mkuu ajiuzulu kwa kushindwa kunda Serikali