Waziri wa Madini, Angellah Kairuki amesema kuwa serikali itaendelea kuwajengea mazingira wezeshi wachimbaji wadogo, kutenga maeneo zaidi kwaajili yao na kuwapa kipaumbele lengo likiwa kuwawezesha, ili washiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi na sekta ya madini kwa ujumla.

Kairuki amewataka wanawake wachimbaji wa madini nchi, kuendelea kuwekeza katika kuongeza thamani madini ya chumvi,kwa kuendana na mahitaji ya soko la ndani, “mkiwekeza katika eneo hili la uongezaji thamani madini ya chumvi mtanufaika na fursa hii, hali itakayosaidia kukuza uzalishaji na kuongeza mchango wa eneohili katika maendeleo ya Taifa letu”

Waziri Kairuki amezungumza hayo jijini Dodoma jana wakati akifungua mkutano Mkuu wa Chama cha Wanawake wachimbaji Madini Tanzania (TOWAMA)

Aidha amewaasa wachimbaji hao wasisite kufika katika ofisi za Wizara ya Madini ,kupata ushauri wa kitaalamu pale wanapokwama katika utekelezaji wa majukumu yao ya uchimbaji wa madini ili kujenga uwezo.

kwa upande wake, Mwnyekiti wa chama hicho Aunice Negele, amesema chama hicho kinaunga mkono juhudi za serikari kupambana na utoroshaji wa madini, iliyaweze kuwanufaisha wananchi wote.

Mfahamu Wilhelm Bleek aliye linganisha sarufi za Kibantu na kuziunganisha
Lowassa atoboa anavyoisubiri 2020, kuhusu kumsifu JPM