Wanawake wengi wajawazito wametajwa kuwa wahanga wakubwa wa matatizo ya kinywa kutokana na mabadiliko ya homoni za kimwili.

Akizungumza na Dar24Media kwenye mahojiano kupitia kipindi cha Afya Tips, mtaalamu wa afya ya kinywa Daktari Winfred Mgaya amesema moja ya tatizo wanalolipata wajawazito ni kuvimba fizi za meno na kutoa damu.

Aidha, Dkt Winfred amesema hali hiyo ya fizi mara nyingi inaanza katika kipindi cha muda wa miezi minne ya kwanza ua ujauzito.

“Kutokana na mabadiliko ya mwili wanawake wengine hawawezi kupiga mswaki vizuri unakuta akiwa anapiga mswaki anatapika sana kwahiyo anaweza akawa anaepuka kupiga mswaki ili asitapike kwa sababu hiyo wanakuwa wahanga wa matatizo ya kinywa,” amesema Dkt. Winfred.

Amesema ili kuweza kuondoa harufu ya kinywa, wanachotakiwa kufanya ni kufanya usafi wa kinywa kwa njia sahihi ambayo ni kupiga mswaki vizuri kwa kutumia dawa yenye madini ya fluoride, uzi maalum wa kusafishia meno, kutumia vitakasa kinywa maalumu na pia kujiepusha na kula vitunguu vya aina zote.

Aidha, ameshauri kuwa ni vyema kwa wanawake wajawazito kuhudhuria Kliniki za meno katika kipindi chote cha ujauzito ili kupata elimu sahihi ya utunzaji kinywa.

CAG mstaafu atema cheche
Rais Samia apokea ujumbe wa Kenyatta, aalikwa rasmi