Wanasiasa wawili wanawake nchini  Ufaransa, Marine le Pen na Anne Hidalgo wamezindua kampeni zao kwaajili ya kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa  kufanyika mwaka ujao.

Marine le Pen kutoka chama cha National Rally  na meya wa Paris  Anne Hidalgo wa chama cha Socialist, sasa wamejitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro hicho.

Hidalgo mwenye umri wa miaka 62, ambaye amekuwa meya wa Paris tangu 2014 ana uwezekano mkubwa wa kushinda uteuzi wa chama cha Socialist amesema  kwamba anapenda kuona watoto wote nchini Ufaransa wanapata nafasi sawa na alizopata yeye katika maisha yake kama mtoto wa wahamiaji kutoka Hispania.

LePen mwenye umri wa miaka 53, ameanzisha kampeni kwenye mji wa kusini wa Frejus ameahidi kulinda uhuru wa Ufaransa. Wawili hao sasa wanaingia kwenye orodha kubwa ya wagombea akiwemo rais wa sasa Emmanuel Macron.

Macron mwenye umri wa miaka 43 bado hajatangaza nia yake ya kuwania urais, ingawa anatarajia kufanya hivyo hivi karibuni. Ushindani mkubwa kwenye zoezi hilo unatarajiwa kuwa kati ya Le Pen na Macron sawa na ilivyokuwa wakati wa uchaguzi wa rais wa 2017.

Makubaliano ya IAEA na Iran yaleta matumaini ya mazungumzo ya mkataba wa nyuklia
Rais Samia avunja mwiko wa Mgawanyo wa Majukumu kijinsia