Mwigizaji mahiri wa filamu kutoka nchini Ghana Majid Michel amepaza sauti akiutaja ukubwa na maajabu ya Mungu kutokana na namna alivyowaumba wanawake na thamani aliyompatia huku akibainisha wazi kuwa wanawake ni toleo bora zaidi kuliko wanaume.

Wakati akijaribu kuelezea sababu za ziada za kauli yake hiyo, mwigizaji huyo ametumia mfano wa matoleo ya simu za mkononi na maboresho yake kwa kusema kuwa “matoleo ya simu yaliyoboreshwa hayawezi kuwa sawa na zile za awali”.

Majid amesema hayo huku akihusisha kauli hiyo na hadithi ya uumbaji kutoka katika kitabu cha Biblia kuhusu Adamu na Hawa/Eva inayosema mwanamke alikuwa wa pili kuumbwa na Mungu baada ya Adamu.

“Nadhani sehemu inayovutia zaidi ya mwanamke ni ubongo wake, Ikiwa Apple watatengeneza simu (iPhone) na baada ya muda wakaamua kuja na toleo jipya, basi hilo toleo jipya, litakuwa juu zaidi na bora kuliko lile la awali.

Mungu alimfanya mwanamume kwanza na akamfanya mwanamke wa pili. Kwa hiyo wanawake ni wa kisasa zaidi wenye akili na nguvu zaidi kuliko sisi. Inanivutia kujua mengi juu ya wanawake, Nawapenda wanawake kuliko vitu vyote” amesema Majid.

Aidha mwigizaji huyo ambaye kwa sasa anajihusisha zaidi na shughuli za uinjilisti ameendelea kumwaga sifa za umahiri wa mwenyezi Mungu kwenye namna alivyowaumba wanawake kiasi cha kuchambua kiwango wanachohusika katika hatua za maisha binadamu.

“Mungu aliposema kuwa nitakufanyia msaidizi, unaonaje?, Je, nikitaka kuinua Meza na ninahitaji msaada, nitahitaji mtu dhaifu kuliko mimi au mwenye nguvu kuliko mimi?, au ninafanya kazi nyumbani, nahitaji msaada hata wa kimawazo, ninahitaji mtu asiye na akili kweli?.

Hapana! Kwa hiyo ikiwa Mungu alisema nitakupa msaidizi basi ina maana anakupa mtu mwenye akili zaidi ambaye anaweza kukusaidia maishani. Wanawake ni bora na wameendelea zaidi,” aliongeza Majid

Unakubaliana na Majid kwa kiwango gani?

Mgodi wa Shanta kuanza kuzalisha Dhahabu 2023
Kim Kardashian akiri ugumu wa maisha bila Kanye West