Wanawake, wametajwa kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili Mashariki na Pembe ya Afrika wakiwa ni asilimia 50.4 ya wahamiaji wote, ikilinganishwa na Wanaume, ambao ni asilimia 49.6, na kufanya upekee katika ukanda huo.

Kwa mujibu wa takwimu za kikanda zilizotolewa katika ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji (IOM) jijini Nairobi, Kenya imesema wakati uhamiaji katika maeneo mengine ya bara unawahusisha wanaume zaidi, ripoti yenye jina A Region on the Move 2021, inaonesha wanaume na wavulana wana asilimia 49.6 pekee katika Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika.

Ripoti hiyo, inaonesha karibu asilimia 60 ya idadi ya wahamiaji katika eneo hilo ni wakimbizi na wanaotafuta hifadhi na Wanawake wanaoongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na wanaotafuta hifadhi, kutokana na uwezekano wa kuhamishwa kwa nguvu, wakati wanaume wana uwezekano wa kuhama kawaida wakitafuta ajira.

Kwa ujumla, mmoja kati ya wahamiaji wanne katika bara la Afrika anaishi katika eneo hilo, ambapo IOM inaeleza kuwa mizozo na ukosefu wa usalama vinasalia kuwa vichochezi vikubwa vya watu kuhama katika eneo hilo.

Aidha imesonesha kuwa, “Kulikuwa na watu milioni 13.2 waliohamishwa kwa lazima katika eneo hilo mwaka 2021, wakiwemo wakimbizi wa ndani, IDPs, milioni 9.6 na wakimbizi milioni 3.6 na wanaotafuta hifadhi.”

Ukame nchini Somalia, Ethiopia na Kenya umekuwa sababu kuu inayochochea uhamaji wa watu katika eneo hilo ukitajwa kuwa ni mbaya kuwahi kutokea katika miongo minne ukisababisha njaa mwaka 2010-2011 na dharura ya ukame 2016-2017 Pembe ya Afrika.

Huduma uokozi wa Maisha zahitaji Dola Mil. 68
'Makanjanja' wa Tumbaku wakalia kuti kavu