Shirika la Umoja wa Mataifa la afya Ulimwenguni (WHO), limesema takwimu zinaonesha kuwa, takriban Mwanamke mmoja kati ya watano atapata tatizo la afya ya akili wakati wa ujauzito au mwaka mmoja baada ya kujifungua na kusema ipo haja ya kusaidia watoa huduma za mama na mtoto kutambua dalili za matatizo ya afya ya akili na kuyapatia ufumbuzi

Kutokana na sababu hiyo, WHO hii leo Septemba 20, 2022 imezindua mapendekezo mapya kwa mamlaka za afya duniani kote, ili kusaidia kuboresha maisha ya wanawake na kusema wakati huu unaweza kuwa ni kipindi cha kuwa na afya mbaya ya akili au kusababisha kuzorota kwa hali ya awali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa WHO, imeeleza kuwa nyakati za kubadilisha maisha kama vile wakati wa ujauzito, kujifungua, na katika hatua za awali za uzazi zinaweza kusababisha mafadhaiko kwa wanawake na wenzi wao huku ufumbuzi huo ukitarajia kutolewa kulingana na mazingira husika ya waathiriwa.

Kazi, kujishughulisha, kula kwa wakati, mazoezi na kuzingatia utimamu wa mwili huepusha maradhi. Picha na UN.

Taarifa hiyo ya WHO imezidi kufafanuwa kuwa, “Na kama hiyo haitoshi, kati ya wanawake walio na hali ya kuumwa afya ya akili wakati wa kujifungua, kabla na muda mfupi baada ya kujifungua karibu asilimia 20 watapata mawazo ya kujiua au kufanya vitendo vya kujidhuru.”

Aidha, imebaimnisha kuwa kupuuza afya ya akili huhatarisha afya na ustawi wa jumla wa wanawake, lakini pia huathiri ukuaji wa mwili na mihemko kwa watoto wachanga, huku ikitoa mwongozo mpya wa kujumuisha afya ya akili ya uzazi katika huduma za afya ya uzazi na mtoto.

Mwongozo huo, pia unaunga mkono huduma zingine, ikiwa ni pamoja na uchunguzi na udhibiti wa kabla ya kujifungua na baada ya kujifungua, Afya ya uzazi kwa mama na mtoto kwa kuangazia mfumo wa Matunzo na Malezi, na utunzaji wa mama na mtoto mchanga kwa uzoefu mzuri baada ya kujifungua na kuboresha maendeleo ya ukuaji wa mtoto.

Kagere, Ndemla kuikosa Geita Gold
Uingereza 'yakuna kichwa' mgogoro wa kiuchumi