Mji mmoja nchini Uganda umewapiga marufuku wanawake kukaa kwenye viti vya mbele karibu na dereva kufuatia misururu ya ajali.

Gazeti la Daily Monitor limeripoti kuwa uamuzi huo ulifikiwa baada ya ajali ya Januari 10 iliyoangamiza maisha ya watu tisa na kujeruhi 19 na maafisa wa usalama mjini Lira, walisema hatua hiyo inalenga kupunguza ajali.

Kutokana na ajali hiyo wanawake wamelaumiwa kuwa chanzo kwa kuaminiwa kuvaa nguo fupi na kuwachanganya madereva wa lori, na hivyo kuchangia ajali.

Mwenyekiti wa Chama cha Wachuuzi wa Soko la Mji wa Lira, Patrick Opio Obote, alisema baadhi ya wanachama waliovalia visivyo walitaka kuketi katika kiti cha matanboi.

“Ili kupunguza ajali, tumeazimia kwamba kuanzia Jumatatu, Januari 17, hakuna mwanamke atakayeruhusiwa kuketi mbele ya lori lolote linalosafirisha wafanyabiashara kutoka Lira City hadi soko lolote la kila wiki,” alisema.

“Wanawake hawa huwa wanavaa nguo fupi. Kila wanapofika kwenye masoko ya kila wiki ya vijijini, huwapeleka madereva kwenye baa ambako huwapa vinywaji na chakula,” alisema Dorcus Adongo, ambaye ni mchuuzi katika soko hilo, alisema wanawake hao hugombania kukaa kiti kilicho karibu na dereva.

Msemaji wa Chama cha Wasafirishaji wa Lira Mjini Bernard Anyeko Matsanga alisema sheria hiyo itafuatwa hata na wake za madereva. “Hakuna mwanamke anayeruhusiwa kukaa mbele na dereva, hata kama wewe ni mke wa mwenye gari, hatukuruhusu,” alisema.

BREAKING: CCM yampitisha Dkt. Tulia pekee uspika wa Bunge
Waziri Bashungwa ateta na Tume ya Walimu