Katika kuhakikisha ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi unaongezeka, wanawake wenye ndoto za kugombea uongozi wameshauriwa kuanza kujifunza kutoka kwa wanawake wanasiasa waliowatangulia, ili kuongeza ujasiri na uthubutu wa kukabiliana na vikwazo kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

Ushauri huo umetolewa na wanasiasa wanawake wakongwe katika mkutano wa jukwaa la wanawake na uongozi lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari WanawakeTanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), na Ubalozi wa Norway kwa lengo la kuwaunganisha wanawake wanasiasa kutoka vyama mbalimbali vya siasa Pemba kubadilishana uzoefu.

Mwana Masoud Ali, mbunge na mwakilishi mstaafu wa chama cha Wananchi CUF jimbo la Mtambwe Pemba alisema, ili wanawake wenye nia ya kugombea waweze kufanikiwa kiuongozi  ni lazima watenge muda kujifunza kutoka kwa wanawake waliowatangulia kuwaelekeza namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake wengi wanapojitokeza kugombea.

Alifahamisha kuwa wanawake wanapojitokeza kugombea nafasi za uongozi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye jamii kutokana na mfumo dume uliojengeka hivyo inahitaji utayari wa wanawake kujiandaa mapema kukabiliana na vikwazo hivyo bila kukata tamaa.

Ishu ya Neymar kumbe ni uzushi mtupu
Young Africans yajiamini kimataifa