Kukiwa na tetesi za kilimanjaro Music Award kutofanya tendo la utoaji wa Tuzo za Muziki  kwa mwaka huu kutokana na waandaji kuboresha malalamiko ambayo yameonekana kujitokeza na kulalamikiwa na watu wengi,Inaelezwa kuwa  waandaji wa tuzo za Oscar wametangaza kuwaalika wanachama wapya zaidi kupiga kura ya maamuzi ya washindi wa mwaka huu

oscars_design_video

Waandaji wa tuzo hizo wamesema  kuwa wamewaalika wanachama wapya zaidi kupiga kura ya maamuzi ya washindi wa mwaka huu, baada ya malalamishi makubwa ya mwaka uliopita ambapo walilaumiwa kwa kuyabagua makundi mengine ya watu.

Waandalizi hao wa The Academy of Motion Picture Arts and Sciences wanasema wamewaalika karibu watu 700, wakiwalenga hasa wanawake na watu kutoka jamii za watu wachache.

Miongoni mwa wale ambao wamealikwa kushiriki katika uteuzi wa washindi wa tuzo hizo ni wacheza filamu weusi, na vilevile waigizaji weusi kutoka Uingereza Idris Elba na John Boyega.

Wachezaji filamu kadhaa wa Hollywood walisusia sherehe za tuzo hizo mnamo mwezi Februari kwa sababu walioteuliwa katika tuzo hizo, hakuwemo mtu kutoka jamii za watu wachache.

Dhofar SC Yamalizana Na Mshambuliaji Elius Maguli
N’Golo Kanté Atengewa Pauni Milioni 25