Hatimae kocha mkuu wa Mwadui FC Ally Bushiri ametangaza idadi ya wachezaji atakaowasajili kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu ya soka Tanzania bara ambao umepangwa kuanza mwezi Agusti mwaka huu.

Bushiri amesema anatarajia kufanya usajili wa wachezaji wanne ambao wakati wowote kuanzia sasa wataanza mazungumzo na viongozi wa Mwadui FC ili kufanikisha maslahi yao binafsi kabla ya kusaini mikataba ya kuitumikia klabu hiyo ya mkoani Shinyanga.

“Binafsi nimeshazungumza na hawa wachezaji, na kilichobaki ni kuwafikisha kwa viongozi ili wakamilishe maswala yao binafsi na kusajiliwa rasmi, naamini watanisaidia katika mipango yangu ya msimu ujao.

“Bila kuwataja majina, nimezungumza na kipa na kiungo mkabaji kutoka Zanzibar, pia nimezungumza na kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wa kati kutoka Tanzania bara.” Amesema Bushiri

Katika hatua nyingine Ally Bushiri ametoa wito kwa makocha wa soka wa visiwani Zanzibar kuanza kutanua wigo wa fikra za ukufunzi wao kwa kuangalia uwezekano wa kutoka visiwani humo na kwenda Tanzania bara kuendeleza taaluma zao.

Bushiri amesema anaamini inawezekana kwa makocha wa Zanzibar kuzinoa klabu za ligi daraja la kwanza la ligi kuu Tanzania bara kama ilivyo kwa wachezaji wa visiwani humo ambao kila msimu wamekua wakipata bahati ya kusajiliwa.

R.Kelly atambua uwepo wa Davido, afanya nae Remix
Juan Antonio Pizzi: Bravo Ni Shujaa Wetu