Polisi katika jimbo la Zamfara kaskazini magharibi mwa Nigeria wanasema wamewakamata watu wanne wanaodaiwa kuhusika na ulaji nyama za watu na kuuza sehemu za binadamu jambo ambalo ni nadra sana katika eneo hilo.

Kamishna wa polisi katika jimbo hilo Ayuba Elkanah akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu Gusau amesema washukiwa hao walikamatwa baada ya maafisa wa upelelezi kupata maiti katika jengo ambalo halijakamilika huku baadhi ya sehemu za mwili zikiwa zimetolewa.

Ilikuwa ni katika harakati za kufanya uchunguzi wa kupotea kwa mvulana wa miaka tisa. Washukiwa hao wakiwemo wanaume wawili na wavulana wawili walikamatwa wiki iliyopita, kulingana na mkuu wa polisi, na kwamba washukiwa wengine wa genge hilo wanasakwa.

Mkuu huyo wa polisi amesema hadi sasa uchunguzi umebaini kuwa mara mbili kiongozi wa genge hilo aliwalipa washukiwa wengine watatu kiasi cha Naira Laki Tano (sawa na $1,207) kwa ajili ya sehemu za binadamu.

Hata hivyo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari Alhamisi kamishna wa polisi Ayuba Elkanah alisema vikosi vya usalama pia vimewaokoa watu kumi na saba waliotekwa nyara hapo awali kutoka jimbo jirani la Niger na kupelekwa Zamfara.

Ahmed Ally: Mbeya City mjipange
Chama kuvaa 17, Sakho namba 10