Wachezaji Peter Banda, Henock Inonga Israel Mwenda na Mosses Phiri hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kitakachoshuka Dimbani leo Jumatano (Januari 18).

Simba SC itakua nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kuikabili Mbeya City FC, katika mchezo wa Mzunguuko wa 20 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambao rasmi utaanza saa moja usiku.

Taarifa kutoka Simba SC imeeleza kuwa Wachezaji hao wanne hawana utimamu wa mwili, baada ya kuuguza majeraha.

Wakati huo huo Simba SC imepangwa kuutumia mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City kuwatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa kupitia Dirisha Dogo, kwa Mashabiki wake watakaojitokeza Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Wachezaji hao ni Mshambuliaji Jean Baleke (DR Congo)Kiungo Ismael Sawadogo (Burkina Faso) na Mshambuliaji Mohamed Mussa (Tanzania).

Mfumuko wa bei kushuka kwa asilimia 1.4
Mwambusi afunguka kuondoka Ihefu FC