Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amethibitisha kutokea kwa ajali ya basi la Kampuni ya Sauli katika eneo la Picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani ambapo watu wanne wamejeruhiwa na wengine 40 wamenusurika.

Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amesema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa anajaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na baada ya kufanikiwa aliona lori la mchanga ndipo aliamua kulikwepa.

Ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021 baada ya dereva wa basi hilo kulielekeza pembezoni mwa barabara ili kukwepa kugongana uso kwa uso na lori lillokuwa likitokea mbele yake.

“Alikuwa anaovateki gari lililokuwa mbele yake na baada ya kulipita aliona lori linakuja mbele yake akalielekeza pembezoni mwa barabara basi hilo na likachegama,”Amesema Kamanda Nyigesa

Majeruhi wamewahishwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi ambapo wamepatiwa matibabu kisha kuruhusiwa.

Rais Samia kuhudhuria uapisho wa Rais Hichilema
Taliban watoa onyo kwa Marekani