Abiria 35 na wahudumu 12 wamenusurika kifo baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria kukosea njia na kuanguka katikati ya Bahari ya Pacific katika Kisiwa cha Micronesia.

Abiria wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo ya Shirika la Ndege la New Guinea (Air Niugini), ANG73 aina ya Boeing 737 – 800 wamepelekwa hospitalini kwaajili ya uchunguzi na matibabu.

Aidha, imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali na hali ya hewa kubadilika ghafla ambapo ilianza kunyesha mvua kubwa muda mfupi baada ya kupaa, jambo lililosababisha ndege hiyo kupotea njia na ilipojaribu kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Chuuk, ilianguka baharini.

Hata hivyo, baada ya ajali hiyo kutokea na ndege kuanguka baharini, abiria na wahudumu wa ndege hiyo walipitia mlango wa dharura.

Maoni hasi kazini: Namna ya kukabiliana nayo kwa ufanisi
Lady Jaydee atamani kunywa sumu