Nchini Malaysia waokoaji sita wamefariki dunia walipokuwa wana mtafuta kijana aliye zama mtoni alipokuwa anavua samaki.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 alizama katika mto huo wakati akivua samaki na rafiki zake siku ya jumatano.

Kamanda mkuu wa polisi wilaya ya Sepang, Abdul Azizi amethibitisha vifo vya waokoaji hao sita na kueleza kuwa walikuwa wamevaa vifaa vya uokoaji lakini kutokana na mvua iliyonyesha mawimbi yaliongezeka na kasi ya maji vilivyo pelekea kuharibika kwa vifaa hivyo.

Wazamiaji hao walikaa kwenye maji kwa muda wa dakika 30 kabla yakutolewa kwenye maji wakiwa wamepoteza fahamu na baadaye wakafariki.

Kamanda huyo aliongeza kuwa hii ni mara ya kwanza kwa waokoaji sita kufariki wakiwa kazini katika nchi hiyo ya Malaysia.

Zaidi ya watu miatano wamejitokeza kutoa heshima za mwisho kwa waokoaji hao kabla hawajakabidhiwa kwa familia zao.

Waziri mkuu wa nchi hiyo, Mahathir Mohamed ametuma salamu za rambirambi kwa familia zao na kuwataka wawe wavumilivu katika kipindi hiki cha majonzi.

Tabia 10 za kuepuka kuinusuru figo yako
Wimbo wa 'Hela' warejeshwa, Kiba afunguka kisa chake

Comments

comments