Waombolezaji wa Msiba, wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza wameonywa kuwa huenda kukawa na misururu mirefu kuliko inavyotarajiwa, katika kuufikia mwili wa Malkia Elizabeth II katika ukumbi wa Great Hall wa Westminster.

Waziri wa utamaduni wa Uingereza, Michelle Donelan amesema kuna maelfu ya wafariji, na mtu anaweza kusubiri kwa saa 30 mstarini kabla ya kufika Great Hall hivyo ameitaka jamii kujianda kusimama saa nyingi kila siku, na kujiandaa kuihimili hali ya hewa.

Amesema, “Serikali itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha watu waliosafiri kuja London hawana matatizo yoyote na kwamba zaidi ya watu 1,000 watakuwa wakisubiri kwenye mstari kila siku kuwasaidia, maduka yatasambaza viburudisho kwa umma.”

Waziri huyo, ameongeza kuwa vyumba 500 zaidi vimehifadhiwa kwenye barabara inayoelekea katika ukumbi wa Westminster, ili kukidhi mahitaji ya umma.

Wakati huo huo, wanawafalme William na Harry watatembea pamoja nyuma ya jeneza la Malkia kwa miguu, katika maandamano kutoka Buckingham Palace hadi Westminster Hall, ambapo mwili wa Malkia utalazwa.

Ndugu watatu, wa Mfalme Princess Anne, Prince Andrew, na Prince Edward pia watatembea kwenye maandamano huku Camilla, mke wa mfalme , na Catherine, Princess wa Wales, watasafiri kwa gari, pamoja na Sophie, Countess wa Wessex, na Meghan, Duchess wa Sussex.

Minziro awaita mashabiki Azam Complex-Chamazi
Bungeni: Mapenzi, Ushirikina vyatajwa wimbi la mauaji nchini