Wabunge nchini Burundi, wamemchaguwa Bi. Aimée Lorentine Kanyana kuwa mpatanishi wa kitaifa ambapo Jumla ya wabunge 120 walioshiriki zoezi hilo la uchaguzi.

Kati ya Wabunge hao 120 walioshiriki uchaguzi huo, 109 wamepiga kura kuchagua mmoja kati ya wagombea 13 wa nafasi hiyo ya mpatanishi wa Warundi.

Ndani ya Bunge la Burundi jijini Bujumbura. Picha ya TRT.

Aimée Lorentine Kanyana, aliyewahi kuwa waziri wa sheria wa Burundi, ni mtu wa tatu kushikilia nafasi hiyo, baada ya Hayati Mohammed Rukara na Édouard  Nduwimana, ambaye muhula  wake upo ukingoni.

Taasisi ya mpatanishi wa kitaifa, ilianzishwa na Mkataba wa Amani uliosainiwa Agosti 28 mwaka 2020 hapa nchini (Tanzania), jijini Arusha, chini ya usuluhishi wa aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.

Meddie Kagere: Young Africans imeimarika
QATAR yapewa kashfa ya kupanga matokeo