Huko Binalonan Kijiji kinachopatikana kaskazini mwa mji mkuu wa Ufilipino, Manila, kimepiga marufuku watu kufanya umbea amesema kila mtu katika kijiji hiko atawajibika kwa atakayoyasema.

Meya wa mji wa Ramon Guico amesema kuwa sababu kubwa ya kukataza watu kufanya umbea ni kutokana na kusababisha ugomvi mkubwa utokee kwenye kijiji hicho.

Na Kwa mujibu wa sheria atakayekutwa na hatia ya kufanya na kueneza umbea na maneno ya uongo atatozwa faini pesa taslimu peso 200 takribni dola za kimarekani 4 sawa na shilingi 9400 za kitanzania, pamoja na tozo hilo la pesa atapewa adhabu ya kukusanya takataka kwa masaa 3.

Ameongezea kuwa atakayekutwa na hatia ya kufanya umbea kwa mara ya pili atatozwa faini ya pesa taslimu peso 1000 takriban dola 20, faini hiyo itaambatana na kupewa adhabu ya kutoa huduma kwa jamii kwa masaa 8.

Guico alisema kuna umbea wa aina nyingi, lakini katika kijiji hicho kesi nyingi ni za umbea unaohusu mali, pesa na mahusiano.

Guico aliongeza kwamba maeneo ambayo watu wake hawafanyi umbea yana Baraka zaidi, kwa sababu yeye anaamini watu wana kazi za muhimu zaidi za kufanya badala ya kufanya umbea.

Atakayekutwa na hatia ya kufanya umbea kwa mara ya pili atatozwa faini ya pesa taslimu peso 1000 takriban dola 20, faini hiyo itaambatana na kupewa adhabu ya kutoa huduma kwa jamii kwa masaa 8.

Dkt. Mengi alivyotembea peku kusaka utajiri na urithi aliouacha
Mfalme amuoa mlinzi wake na kumpa hadhi ya Malkia