Wagombea Udiwani wa vyama vya CUF, Chadema na Ada-Tadea, wamelalamikia hatua ya msimamzi wa uchaguzi Kata ya Mbagala Kuu, kumtangaza mgombea wa CCM kupita bila kupingwa ingawa wamerejesha fomu kwa mujibu wa sheria.

Hayo yamesemwa na mgombea wa CUF, Abukabar Mlawa, ambapo amesema kuwa hatua ya kutangazwa mgombea wa CCM, Shabani Abubakar ni kinyume na sheria za uchaguzi.

Hapo awali, kata hiyo ilikuwa inaongozwa na Yusuph Manji ambaye aliondolewa kwa mujibu wa sheria baada ya kuonekana ameshindwa kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani kwa muda mrefu.

Amesema kuwa msimamizi wa uchaguzi wa kata hiyo aliwataka wagombea wa vyama mbalimbali kuchukua fomu za kuwania udiwani kuanzia Agosti 17, mwaka huu na kutakiwa kuzirudisha fomu hizo jana saa 10:00 jioni.

Aidha, ameongeza kuwa ilipofika saa 5:00 asubuhi jana, yeye pamoja na wagombea wa vyama vingine wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ACT-Wazalendo na CCM, walirudisha fomu hizo lakini ilipofika saa 10:00 jioni walikuta msimamizi huyo ameshampitisha mgombea wa CCM.

Kwa upande wake mgombea wa Chadema, Muganyizi Emanuel amesema kuwa walirudisha fomu saa 5: 00 asubuhi wakati muda uliotangazwa wa mwisho ni saa 10:00 jioni, lakini walishangazwa na kitendo cha msimamizi msaidizi wa uchaguzi kumpitisha mgombea bila ya kufuata sheria.

Weah ampa tuzo Arsenal Wenger
Video: Mimi napambana kwaajili ya Rais Dkt. Magufuli tu- Musiba