Israel inalazimika kufanya uchaguzi mwingine mwezi Septemba mwaka huu, baada ya wabunge kupitisha hoja ya kulivunja bunge kufuatia Waziri mkuu, Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda serikali ya muungano.

Bunge la Israel Knesset jana lilipiga kura 74 dhidi ya 45 za kuunga mkono hoja ya kuvunjwa kwake na kuitishwa uchaguzi utakaofanyika Septemba 17, ambapo Netanyahu ambaye ameiongoza Israel kwa muongo mmoja uliopita, alionekana kuongeza muhula wa nne madarakani lakini alishindwa kuafikiana na washirika wake na hususani juu ya muswada unaopendekeza ulinzi wa Netanyahu dhidi ya tuhuma za rushwa.

Chama cha Likud cha waziri mkuu Netanyahu kiliona bora kuwasilisha hoja ya kuvunjwa bunge ili ufanyike uchaguzi mpya ambao unakuwa wa pili ndani ya mwaka huu. ambapo Netanyahu amesema kuwa taifa hilo linalazimika kuingia katika uchaguzi ambao haukuhitajika lakini anaamini chama chake kitaibuka na ushindi.

“Tutafanya uchaguzi wa mapema, na kampeni za wazi zitakazotupatia ushindi. Tutashinda!, tutashinda na umma utashinda. Ni vigumu kuamini kwamba, Avigdor Lieberman sasa yuko upande wa kushoto. Avigdor Lieberman yuko upande wa kushoto, amesema Netanyahu

Aidha, nchi hiyo sasa inaingia katika kampeni za uchaguzi mpya ambazo zitadumu kwa muda wa miezi mitatu chini ya sheria ya Israel, ambapo Netanyahu amekuwa na mazungumzo ya takribani wiki sita bila ya mafanikio na chama cha waziri wa zamani wa ulinzi, Avigdor Lieberman cha Yisrael Beiteinu na kile cha Kiyahudi cha Utra-Orthodox.

Hata akishinda uchaguzi ujao bado uwezekano wa kuunda serikali ya muungano ni mdogo na hivyo kulazimika kukubaliana na matakwa ya kisiasa ili kuungwa mkono yatakayomlazimu kusimama mahakamani kwa tuhuma za rushwa.

Sitarajii kugombea wala kurudi Jimboni kwangu- Nyalandu
Fedha za vitambulisho vya JPM zawatokea puani