Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa viongozi wa vyama vya upinzani watapata tabu kwakuwa wanashindwa kusimama katika itikadi zao na kuhitaji huruma kwa wananchi.

Amesema kuwa wapinzani wanashindwa kutimiza wajibu wao na kusimamia migogoro ndani ya vyama vyao, matokeo yake wanasingizia kuonewa na CCM.

”Kusema wanaotoka upinzani kuhamia CCM, wananunuliwa ni kutafuta huruma, mwaka 2010 Mawaziri wakuu wastaafu wawili (Edward Lowasa na Frederick Sumaye) waliondoka CCM lilionekana ni jambo jema ila leo wanapokuja kwetu linakuwa jambo baya huo ni unafiki wa kisiasa,”amesema Polepole

Aidha, ameongeza kuwa hakuna mbunge anayenunuliwa kuhamia CCM ila ukweli ni kwamba akitaka kuunga mkono juhudi za Rais hawezi kuunga akiwa upinzani lazima atakuwa mnafiki ndio maana wanaenda CCM ili wawe huru.

Hata hivyo, mpaka sasa jumla ya wabunge wanne kutoka vyama vya upinzani wamekwisha jiunga na CCM wakiwemo watatu kutoka Chadema na mmoja kutoka CUF huku Madiwani wakiwa zaidi ya 50 wamejiunga na CCM.

 

 

 

Maswali 10 yanayoulizwa mara kwa mara kwenye 'Interview'
Moise Katumbi apokelewa kwa shangwe katika mji wa Kasumbalesa