Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro amesema kuwa vyama vikubwa vya upinzani nchini humo vimezuiwa kushiriki kwenye uchaguzi ujao wa urais ambao unatarajiwa kufanyika mwaka 2018.

Maduro amesema kuwa vyama pekee ambavyo vitashiriki ni vile ambavyo vimeshiriki kwenye uchaguzi wa meya uliofanyika Jumapili iliyopita, ambapo vyama vikubwa vilisusia.

Aidha, amesisitiza kuwa mfumo wote wa uchaguzi nchini humo ni wa kuaminika, na kwamba vyama hivyo vilivyosusia uchaguzi vimejipoteza kwenye ramani ya siasa.

“Chama ambacho hakijashiriki kwenye uchaguzi huu hakitashiriki tena, kwani wamejiondoa kwenye ramani ya siasa,” amesema Rais Maduro

Hata hivyo, Viongozi wa vyama vya Justice First, Popular Will na Democratic Action walisusia uchaguzi wa meya, wakisema kwamba mfumo wa upigaji kura sio wa haki

Shangwe za Man City zamkera Mourinho
Netanyahu: Jerusalem ni mji mkuu wa Israel