Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaibuka na ushindi katika Jimbo la Buyungu lililopo mkoani Kigoma, hivyo wapinzani wasipoteze muda wao bure.

Amesema kuwa takwimu za tathmini ya maendeleo ya kampeni jimboni Buyungu zinaonyesha kuwa CCM inaongoza kwa mvuto miongoni kwa wapiga kura na kwamba huenda chama hicho kikashinda kwa zaidi ya asilimia 70.

Aidha, Nape amewataka viongozi wa vyama vya upinzani na wagombea wao kuzungumza kwa takwimu wanapoeleza mafanikio ya mambo yaliyofanywa na wabunge wao badala ya kupiga makelele na kuwadanganya wananchi na kwamba wakati wa wapinzani kupiga kelele na kudanganya wananchi umekwisha.

 

Wanafunzi 9 wafariki nchini Kenya
Majaliwa akunwa na Makumbusho ya Taifa

Comments

comments