Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Deo Ndejembi amesema Serikali imetoa maelekezo kwa waratibu wa Maendeleo ya Jamii TASAF kuanzisha vikundi vinavyotokana na kaya masikini ili viweze kunufaika na mikopo ya asilimi 10 ambayo imekuwa ikitolewa kote nchini.

Amesema hayo wakati na Waratibu wa TASAF mkoa wa Ruvuma, ambapo amewapa muda wa mwezi mmoja kuhakikisha kila mmoja anaanzisha vikundi viwili vinavyotokana na mfuko huo.

Ndejembi amesema TASAF ni miongoni mwa mifuko mikubwa inayogusa maisha ya watanzania wanaotoka kaya maskini, hivyo ni vema waratibu wa TASAF nchini wakaacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake waongeze ubunifu ili kuzinyanyua kaya masikini.

“Huu mradi ni mkubwa ambao Serikali yetu inautazama, na tena mwaka huu tumeongeza maeneo katika kipindi hiki cha awamu ya Sita kinaanza ambapo hakuna kijiji wala kata itaachwa, kote huko tumelenga kuwafikia walengwa wa TASAF ili waweze kunufaika na fedha zinazotolewa na Serikali yao.”amesema Naibu Waziri Ndejembi

Pia ameipongeza TASAF kwa kuingia mkataba na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), mkataba ambao utawasaidia Wanafunzi wanaotoka kaya maskini kupata mikopo ya kujiendeleza kielimu.

Serikali kuja na mpango wa kukabiliana na maafa
Tetemeko la ardhi laua watu 20 Pakistan