Wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya nchini wameipongeza kampuni inayozalisha Konyagi kwa kuwapa fursa ya kuthamini ujasiri, ushupavu na uthubutu wa wanawake ambao wamejitoa katika kazi zao za kimuziki na kuwajenga katika Maisha kiujumla baada ya Konyagi kutoa chupa yenye nembo maalumu ya mwanamke aliyeinua mikono kama kiashiria cha kutambua umuhimu wa mwanamke katika jamii.

Mmoja wa wasanii hao, John Simon Mseke maarufu kama Joh Makini, ameishukuru Konyagi kwa fursa iliyompa ya kumzungumzia mwanamke ambaye anaamini amekuwa na mchango mkubwa katika maisha yake na amesema mama yake mzazi ndio kila kitu kwake na anabaki kuwa mwanamke wa nguvu katika maisha yake.

‘Siwezi kumaliza maneno nikiamua kumzungumzia mama huyu shupavu, mimi mwenyewe ni mzazi pia, hivyo najua changamoto alizopitia mama yangu wakati nikiwa tumboni, aliponizaa na wakati akinilea, amesema Joh makini.

Naye Juma Musa maarufu ‘Jux’ amesema mama yake amekuwa na mchango mkubwa katika safari yake ya kimuziki iliyokuwa na vikwazo vingi vya kukatisha tamaa, huku akiweka bayana kuwa wakati anaanza muziki kuna watu wa karibu waliokatisha tamaa wakiwemo wa familia yake, lakini mama yake alimwambia anaweza.

“Mama alinifundisha maisha, namna ya kuwajali wanawake wengine na watu wote wanaonizunguka. Licha ya kuwa peke yake, alinipa malezi bora na kunilea,” ameongeza Jux.

Siku ya Wanawake Duniani imegusa kila mtu duniani kutokana na mchango wa wanawake hasa mama, sio tu katika malezi na kujenga familia bora bali pia kushiriki shughuli za kiuchumi na shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na wanaume kama vile udereva, ufundi na nyinginezo nyingi.

Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.

Kaze arudisha 'KOMBORA' Young Africans
Prince Dube aumia tena Azam FC