Watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kupora kiasi cha shilingi milioni 464.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi ambapo amesema kuwa watu hao walikamatwa, Agosti 3 na  Julai 19 mwaka huu mkoani Singida walipokuwa wamekimbilia mara baada ya kufanya uhalifu.

Amesema kuwa watu hao walikamatwa na fedha halali za Kitanzania Sh.40 milioni na Dola za Marekani 190,000 na silaha aina ya Short gun vilivyoibiwa katika kiwanda kinachojihusisha na biashara ya mabondo ya samaki cha Weish AST Ltd cha jijini Mwanza.

Aidha, Kamanda Msangi amewataja watu hao kuwa ni Seif Waziri (37), Daud Mwakalinga (35) wote wakazi wa Dodoma waliokamatwa wakiwa mkoani Singida wakiwa wamebaki na Sh.2 milioni na Dola za Marekani 20,000.

“Baada ya mahojiano ya awali walipoletwa Mwanza, majambazi hao walikiri kuhusika na tukio hilo kisha walionyesha walipokuwa wameficha silaha na kumtaja mwezao amabaye naye alikamatwa,” amesema Kamanda Msangi

  • Mwakyembe awang’ata sikio wasanii, awapa siri ya mafanikio

    Vile vile, amesema kuwa watu hao walikutwa na silaha aina ya shortgun yenye namba 011765714 na car namba 00107210 vitu vilivyoporwa jijini Mwanza. Mwingine ni Emmanuel Mwakilili aliyekamatwa jijini Mwanza baada ya kutajwa na wenzake.

  • Mpina atoa mwezi mmoja kukamilishwa kwa mradi wa maji

    Hata hivyo, Kamanda Msangi ameongeza kuwa tukio hilo la uporaji lilitokea jijini Mwanza Julai 14, mwaka huu ambapo majambazi watano walivamia kiwanda hicho wakiwa na silaha za jadi na kumpiga mlinzi na kitu kizito kichwani na kumpora silaha kisha kuingia ndani na kupora kiasi hicho cha fedha na kutokomea kusikojulikana.

Siku zake zahesabika, amtendea mkewe unyama mbele ya watoto wao
Picha: Wafuasi wa Lipumba na Maalim Seif wanyukana mahakamani