Waalimu wawili waliokuwa wakifanya mazoezi kwa vitendo katika shule ya sekondari ya Kikala wilayani Lushoto mkoani Tanga wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kufanya mapenzi na wanafunzi wawili wa kidato cha tatu shuleni hapo

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, January Lugangika ambapo amesema kuwa waalimu wa wanafunzi hao wamekiuka maadili ya ualimu na kwamba watachukuliwa hatua zaidi huku akiongeza kuwa tabia kama hizo zinaleta kichefu chefu kwa jamii.

“Inabidi wazazi muwafatilie watoto wenu kwa kila hatua, mjue wanafanya nini shuleni na kama mzazi humfatilii anaweza kufanya mambo usiyoyajua na badala yake ukashtukia ana mimba ya miezi hata sita,”amesema Lugangika

Hata hivyo, kwa upande wa Afisa Elimu wa Sekondari Wilaya ya Lushoto, Kassim Singato amesema endapo kutakuwa na masomo ya ziada ni lazima yafahamike muda yanapoisha ili wazazi waweze kufuatilia mwenendo wa watoto wao.

Umoja wa Ulaya waunda mpango wa kukabiliana na wahamiaji haramu
Video: Kichupa cha Patoranking na Diamond Platinumz 'Love you Die'