Wahindi wa Tuzo za Umahiri wa uandishi wa habari Tanzania EJAT 2020 watajulikana leo Septemba 10 katika kilele cha sherehe hizo zitakazofanyika katika ukumbi wa kituo cha kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Wanahabari 59 wameteuliwa kuwania Tuzo hizo ambapo washindi wa Makundi mbalimbali na wa jumla wanatarajiwa kutangazwa

Mgeni Rasmi anatarajia kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais mstaafu Joseph Sinde Warioba.

Kutokana na Janga la Covid 19 waalikwa wa kushiriki sherehe hizo wamepunguzwa na ndugu wa washiriki wataangalia kupitia mtandao.

Katika tuzo hizo Dar 24 Media imewakilishwa na Stanslaus Lambati.

Rais Samia afanya uteuzi
Akaunti za benki kufungwa nchini Guinea