Idara ya Sheria jijini New York nchini Marekani, imesema imewashtaki watu 48 kwa ulaghai dhidi ya programu za kupambana na njaa wakati wa janga la Uviko-19 na kuiba dola milioni 240 baada ya kuilaghai na kuitoza serikali milo ya watoto ambao hawakuwapatia huduma stahiki.

Kesi hiyo, iliyounguruma jijini Minnesota, imesema tukio hilo lilifichuliwa katika mpango wa kukabiliana na janga hilo, huku waendesha mashtaka wakidai, hawatapuuzia kupambana na vitendo vya matumizi makubwa ya serikali na kusema uzembe wa usimamizi viliruhusu kuenea kwa kashfa na uwiano mdogo wa tukio hilo.

Katika operesheni ya Minnesota waendesha mashtaka hao pia walisema, madai ya watuhumiwa hao yalihusisha risiti bandia za milo milioni 125, na wahusika walikuwa na ujasiri kufuatia mtuhumiwa mmoja kuiambia serikali kuwa aliwalisha watoto 5,000 kwa siku katika ghorofa moja la nchini humo.

Jumba la Idara ya haki lililopo jijini New York nchini Marekani. Picha na ABC News.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo, walionekana kuweka juhudi ndogo katika kuficha walichokuwa wakifanya, kwa kutumia tovuti ya listofrandomnames.com, kuunda orodha ghushi ya watoto ambao wangeweza kuwatoza kwa kulisha huku wengine wakitumia programu ya kuzalisha idadi na umri kwa watoto wanaodaiwa kuwalisha.

Hata hivyo, Gazeti la The New York Times mapema Machi 2022 liliripoti kuwa watu hao waliingiza mamilioni ya dola kwa wiki, huku waendesha mashtaka wakisema maafisa wa serikali walikuwa walikosa umakini katika uangalizi wa mpango wa kulisha watoto wakati wa janga hilo kutokana na wahusika kupata msaada wa mtu wa ndani anayeaminika.

Wamemtaja mtu huyo wa ndani kuwa ni Bi. Aimee Bock, ambaye ni mwanzilishi wa kundi lisilo la faida la Feeding Our Future, ambalo Jimbo la Minnesota lilitegemea angekuwa mlinzi wa kukomesha ulaghai kwenye tovuti za kulisha lakini alifanya kinyume chake na alitumia vibaya nafasi yake kuleta karibu shughuli 200 za ulishaji chakula zikiwasilisha ankara bandia.

Viashiria uvunjifu wa amani vidhibitiwe: Majaliwa
Mikoa yenye viashiria vya kigaidi yatajwa