Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imewafutia mashtaka na kuwaachia huru washtakiwa watano waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia bomba la mafuta mali ya Mamlaka ya Bandari (TPA) isivyo halali.

Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 23, 2019 na Hakimu Mkazi mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania DPP kuieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Walioachiwa huru na mahakama hiyo ni Audai Ismail, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.

Inadaiwa mwaka 2015 hadi Januari 8, 2018 katika eneo la Tungi Muungano wilaya ya Kigamboni, washtakiwa hao walijiunganishia bomba la mafuta ya dizeli lenye upana wa inchi moja kutoka katika bomba lenye upana wa inchi 24, bila kuwa na kibali.

Lakini pia walishtakiwa kwa kosa la pili la kuharibu miundo mbinu, ambapo inadaiwa siku hiyo ya tukio, washtakiwa hao walitoboa bomba la hilo, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta,  mali ya Mamlaka ya Bandari nchini( TPA). Pia wanadaiwa kuharibu bomba la mafuta mazito( Crude oil) lenye upana wa inchi 28, ambalo lilikuwa likitumika kusafirisha mafuta ghafi, mali ya Mamlaka ya Bandari nchini( TPA).
Aidha, mapema jana Rais Magufuli ametoa siku 7 kwa washtakiwa wote waliohujumu uchumi kutubu juu ya kosa hilo na kuahidi kutorudia tenaq lakini pia amempa ruhusa DPP kuwasikiliza endapo wataridhia kurudisha mali walizohujumu waweze kuachiwa huru na rasmi utekelezaji wa agizo hilo umeanza leo Jumatatu hadi jumamosi.

Unai Emeri atoa sababu kwa nini Pepe na sio Aubameyang?
Gianni Infantino kula sahani moja na wabaguzi wa rangi